|
Article on other languages:
|
Matunda ni sehemu ya mimea kama miti au vichaka vyenye mbegu ndani yake. Kwa lugha ya biolojia ni sehemu ya ua la mmea katika hali ya kuzaa mbegu. Kwa lugha ya kila siku ni zaidi sehemu hiyohiyo kama ina pande zinazoliwa. Ua la mmea kama imeendelea kukuza mbegu hufunika mbegu mwenyewe kwa ganda la kuukinga. Ganda hili mara nyingi lina sehemu ya nyama ya tunda. Kama sehemu hii ina lishe kwa mwanadamu na ladha ya kupendeza basi ni tunda la kuliwa. Matunda mengi yana maji ndani yake pamoja na sukari asilia. Asilimia kubwa ya tunda ni nyuzi ya kitembwe. Ina kiasi kikubwa cha vitamini na madini kama chuma. Kwa kawaida matunda hayana proteini na mafuta mengi isipokuwa matunda ya pekee.
|
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.