|
Article on other languages:
|
Nafaka ni mbegu wa aina mbalimbali za manyasi. Ni pia jina kwa ajili ya aina za manyasi ambazo mbegu zake zinaliwa kama chakula cha kibinadamu. Manyasi za nafaka ni kati ya mimea muhimu zaidi inayotumiwa kama chakula cha watu duniani. Nafaka muhimu ni pamoja na
Aina tatu za nafaka ambazo ni 87 % za mavuno ya nafaka zote duniani muhindi, ngano na mpunga. Nafaka zina wanga (kabohaidreti) ndani yake ambayo ni lishe muhimu ya watu. Kuna pia kiasi kidogo cha protini. Punje za nafaka zinaliwa baada ya kuzivunja kiasi na kuzilainisha ndani ya maji. Kwa kawaida nafaka huliwa baada ya kupondwa au kusagwa kuwa unga. Ugali, uji, maandazi, chapati, mkate, keki na spaghetti ni mifano ya vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia unga wa nafaka. Marejeo
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.