|
Article on other languages:
|
Herodoti wa Halikarnassos (484 KK hadi 425 KK) alikuwa mwandishi wa historia wakati wa Ugiriki ya Kale. Alikuwa mwenyeji wa mji wa Halikarnassos katika Asia Ndogo (Uturuki ya leo) akasafiri baadaye na kutembelea nchi nyingi. Herodoti ni maarufu kwa sababu alikusanya habari nyingi za historia ya kale ya mataifa ya Asia, Afrika na Ulaya. Waroma wa Kale walimwona kama "Baba wa historia". Sehemu kubwa ya maandiko yake yamepotea yanajulikana tu kwa sababu yanatajwa katika vitabu vingine vya kale. Lakini historia yake ya vita kati ya Wagiriki na Wajemi wakati wa karne ya 5 na 6 KK imehifadhiwa. Kwa jumla hata wataalamu wa leo hutegemea mara nyingi habari zilizokusanywa na Herodoti juu ya Babeli, Misri, Uajemi na Wagiriki wa Kale. Alisafiri akitembelea Italia, Bahari Nyeusi na Misri. Alikusanya habari nyingi kutoka watu wengine pia. |
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.